Wandugu na wadada katika Kristu

Katika muda huu kabla ya wakati kupita kwa milele, kiito kisicho cha dunia kinatualika kuhubiri Neno la Mungu lisilochanganishwa, na pia kutangaza ujumbe uliotumika kwa Kanisa la Laodikia kupitia kwa nabii aliyeitwa ndugu William Marrion Branham. Ujumbe unaita Bibi Arusi wa Kristu kutoka Babuloni Mkuu na kurudi mpaka imani ya mitume ya Bibilia, vile Malaki 4:5 imeandikwa.

Mwenye dhambi, kuja ili utazame, utabadilishwa!

Living Christian Church International (LCCI) ni kanisa ambalo halijalinganishwa na madhehebu yoyote na ambalo halina imani isipokuwa Kristu, bila sheria yoyote isipokuwa Upendo, na bila kitabu kisipokuwa Bibilia. Tunaamini vile mitume waliamini, tunafanya ubatizo vilivile na tunahubiri Injili yenye Paul, Peter na wengine walihubiri miaka elfu mbili iliyopita. Tutabaki na Neno la Mungu lililofunuliwa mpaka Yesu atarudi na kutupokea nyumbani.

Yesu Kristu ni yuleyule, jana, leo na milele. Mungu ameongea na Noa, na mawingu ya mvua yanakaribia. Tuingie katika safina ingawa muda imebaki!
 Mungu awabariki nyinyi nyote.

"...Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na
mchana wala usiku, siku ijulikanayo na BWANA. Jioni inapofika nuru itakuwepo..."

 

Zekaria 14:7 

    

Siku ya Bwana inakuja kwa upesi

Amini letu

  • Ni kwamba Bibilia imeandikwa kwa msukumo wa Roho Mtakatifu, bila makosa yoyote, na kwamba Bibilia imeletwa uhai kwa ujumbe wa wakati wa mwisho.

  • Ya kuwa Mungu ni mmoja, anayejionyesha katika ofisi za Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (Kumbukumbu la Torati 4:35-39; Kumbukumbu la Torati 32:39; 1 Mambo ya Nyakati 17:20; Isaya 43: 10-11; Yohana 14:5-11; Isaya 44:6-8; Ufunuo 1:8; Wakolosai 1:15-20; Marko 12:29-34; Isaya 9:6 na kadhalika.)

  • Ubatizo ni kwa Jina la Yesu Kristu vilevile mitume, baada ya pentekoste wakiwa wamejazwa na Roho Mtakatifu, walifanya kazi ya Mathayo 28:19.  Walifaya ubatizo katika Jina halisi la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, ambalo ni Yesu Kristu, ukifuata maandiko haya: Isaya 9:6, Matendo 2:37-38; Matendo 19:3-5; Waroma 6:3-4; Matendo 8:16; Matendo 4:10-12; Matendo 10:47-48, na khadhalika. (Tafadhali tumia wakati ili utazame maandiko haya. Utabadilishwa!)

  • Ya kwamba ubatizo katika Roho mmoja unatuletea kwa mwili mmoja, ambao ni Bibi Arusi wa Kristu. Na pia kusema ya kwamba Roho Mtakatifu ni muhuri wetu wa ukombozi (Waefeso 4:30.)

Ili upate maandiko mengine kuhusu amini letu, chagua hapa.