eagle in nest_edited.jpg

("Nest" katika Kiswahili inamaanisha "Kiota")

"Nest" ni jaribio letu la kusisimua vijana wetuili waweze kuelewa injili. Kanisa letu inataka kuweka mbegu kwenye moyo ya kila mwaminifu katikati yetu. Tunataka njaa yao ya kusikiliza Neno itimize.

Vijana katika Ujumbe wanafaa kushirika pamoja katika mazingira bila ushawishi wa ulimwengu, na tunawakupa uwezo huu. Wanaweza kutoa ushuhuda wao, maandiko katika Neno na mashauri yao kuhusu Maisha ya mkristo, bila kulaumishwa.

Na je, nabii alisemaje kuhusu vijana?

 

73 Wadumishe kwenye marafiki Wakristo kadiri uwezavyo. Wadumishe pamoja na…Iwapo ni msichana, mweke pamoja na wasichana Wakristo; wavulana Wakristo, vivyo hivyo. Kama msichana amefikia umri wa kutosha kuambatana na mvulana, ona kwamba anaambatana na mvulana mwema. Mshauri asiambatane na mvulana asiyefaa, au mvulana kwa msichana. Kama msichana yule anafanya uchumba na asiyeamini, jaribu kumshauri apozwe na mwamini, na kadhalika. Fanya nyumbani kwako kuzuri. Fanya nyumbani kwako mahali ambapo binti yako na mwanao hawataaibika kuleta wenzi wao mbele ya baba na mama yao, na nyumbani mwao; na fanya nyumbani kuzuri sana hata watafurahia kukaa nyumbani mwao.

    64-0830E - Maswali Na Majibu #4
    Rev. William Marrion Branham

390. Ndugu Branham, ni mafanikio gani ambayo tungewaachilia watoto wetu ambao hawajabalehe kushiriki: (Samahani, ni)—Ni shughuli gani watoto wetu wasiobalehe wanapaswa kutazamia—kushiriki katika shughuli gani. Pia yatupasa tuwasaidieje kuchagua wenzi wao?

" Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake; Na kupapatika juu ya makinda yake, Alikunjua mbawa zake, akawatwaa, Akawachukua juu ya mbawa zake;   Bwana peke yake alimwongoza . . . "

Kumbukumbu la Torati 32:11-12

Nabii William Branham alituelezea ya kwamba hii ni wakati wa tai, na sisi kama tai tunaruka juu ya shida za ulimwengu. Waaminifu katika Bibi Arusi wanapaswa kushauri vijana wao kabla waingie vita ya Bwana. Kwa hivyo, tutawaongoza katika Kiota hiki, na Mungu akichelewa wataweza kuongoza Watoto wao.